Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haondoki kipa wala hatutasajili kipa mpya - Simba

Lakred X Manula Manula na Ayoub Lakred.

Wed, 26 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imesema kuwa haina mpango wa kuligusa eneo la kipa kwenye dirisha la usajili msimu huu kwani makipa waliopo ni wazuri na wanatosha kuitumikia klabu hiyo.

Hayo yamesemwa na meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally wakati akizungumzia usajili mpa msimu ujao.

“Hatuna mpango wa kuongeza kipa mwingine kwa sababu wachezaji kwenye eneo la kipa hatutaligusa kabisa msimu huu hata kidogo.

“Tuna Ayoub Lakred, Aishi Manula, Ally Salim, Abel Hussein, na ferrous Telu, tuna makipa wengi na wazuri, jukumu letu ni kuendelea kuwatunza waendelee kutumikia kwa ubora wao ule ule,” amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live