Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hao Prisons sasa sifa, yainyoosha Namungo Sokoine

Prisons X Namungo Hao Prisons sasa sifa, yainyoosha Namungo Sokoine

Thu, 21 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Tanzania Prisons imeendelea kuwa mwiba katika Ligi Kuu baada ya kuichapa Namungo bao 1-0 na kupanda hadi nafasi ya tisa kwa pointi 17.

Ushindi huo unakuwa wa tatu katika mechi nne alizosimamia kocha mpya, Ahmad Ally kwenye siku 26 alizodumu tangu ajiunge na Maafande hao akichuchukua nafasi ya Fredi Felix 'Minziro'.

Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, ulikuwa wa kasi na upinzani mkali kutokana na kila timu kucheza soka safi kusaka alama tatu na wenyeji kuweza kufanya kweli.

Prisons ilitakata zaidi dakika 45 za kwanza huku Namungo wakibadilika zaidi kipindi cha pili japokuwa mashambulizi yao hayakuwa na faida

Kocha Ally amesema kufanya vizuri ni kutokana na wachezaji kumuelewa anachoelekeza, sapoti ya mabosi na ushirikiano na wenzake kwenye benchi la ufundi.

"Vijana wamenipokea vyema wakaelewa ninachowaeleke, viongozi pia sapoti yao ni kubwa na zaidi benchi la ufundi Tunashirikiana kupanga mambo yote na mwisho tunafanikiwa" amesema Ally.

Kocha wa Namungo, Nsajigwa amesema hawakuzidiwa zaidi na wapinzani isipokuwa bahati iliwabeba kwa kutumia nafasi moja waliyopata bao.

"Kipindi cha kwanza ni kama tulizidiwa lakini hadi mwisho tulikuwa sawa, tulitengeneza nafasi nyingi lakini hatukuweza kuzitumia zaidi ya wao kupata ile nafasi moja wakafunga bao" amesema Nsajigwa.

Licha ya kuonesha kiwango bora, Prisons ndio timu pekee Ligi Kuu iliyotolewa mapema michuano ya kombe la shirikisho la Azam (ASFC) ilipochapwa penalti 6-5 dhidi ya TRA ya First League baada ya dakika 90 kuisha kwa suluhu.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: