Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hansi Flick kocha wa makombe atua Barcelona

Hansi Flick Hansi Flick

Wed, 29 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Barcelona au Barca hatimaye imemteua rasmi kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani, Hansi Flick kuwa kocha mkuu kwa mkataba wa miaka miwili.

Flick ambaye pia amewahi kuwa kocha wa timu ya Bayern Munich pia ya Ujerumani, Septemba mwaka jana alitimuliwa timu ya taifa ya Ujeumani na sasa anachukua nafasi ya Xavi ambaye wiki iliyopita alitimuliwa Barca.

Hadi kuteuliwa kuinoa timu ya taifa ya Ujerumani, Flick alipata mafanikio akiwa na Bayern hasa mwaka 2020 alipoiwezesha kubeba mataji matatu ‘treble’ ambayo ni Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga, Kombe la Ujerumani na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mshambuliaji wa Barca, Robert Lewandowski, 35, anamjua vizuri Flick kwani walikuwa naye katika klabu ya Bayern Munich kwa misimu miwili iliyokuwa na mafanikio.

Mara baada ya kutimuliwa Barca, Xavi alinukuliwa akisema kwamba kocha atakayechukua nafasi yake atapata tabu sana kwa kuwa kazi ya kuinoa timu hiyo ni ngumu na ina mambo mengi.

Mafanikio pekee ambayo Xavi ameyapata akiwa na Barca ni kubeba taji la La Liga msimu uliopita ingawa msimu huu umekuwa mgumu kwake baada ya timu hiyo kumaliza ligi ikiwa nafasi ya pili nyuma ya mahasimu wao Real Madrid kwa tofauti ya pointi 10.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live