Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hans Rafael awashauri Simba cha kufanya

Mangungu Mo Dewji Hans Rafael awashauri Simba cha kufanya

Wed, 29 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rasmi Klabu ya Simba wameshika nafasi ya tatu kwenye ligi nyuma ya mabingwa Yanga SC na Azam FC.

Kwa utamaduni wa timu kubwa kama Simba hii nafasi ya tatu siyo hadhi yao,lakini kusema ukweli hawakuwa na msimu mzuri.

Msimu huu Simba wamefunga goli (59) na kuruhusu goli (25) huku wapinzani wao wakubwa Yanga wakifunga goli (71) na kuruhusu goli (14) Azam wao wamefunga goli (63) na kufungwa (21).

Kwa takwimu hizo ni wazi Simba hawakuwa na wastan mzuri wa kufunga na kuzuia,huku takwimu zikionyesha Coastal Union walikuwa bora kiulinzi kuliko Mnayama kwani wao wameruhusu goli (19) ndani ya msimu mzima.

NINI KIFANYIKE? Simba wanatakiwa kurudi kwenye ubao wao na kuchora upya ramani Simba wanahitaji damu changa zenye quality na uchu wa mafanikio.

Viongozi wa Simba wanatakiwa kuachana na kona kona na mambo ya 10% pesa yote iwekezwe kwa wachezaji wa maana….ni bora usajili wachezaji wachache wenye ubora kuliko lundo la watu wenye uwezo mdogo (tukumbuke timu haijengwi kwa dirisha moja la usajili).

Kwa maoni yangu Juma Mgunda anatakiwa kuheshimika na kupewa muda kwani ana kila sifa ya kuirejesha Simba imara. Kwa bahati nzuri msimu ujao hakuna Champions League hivyo ni wakati sahihi wa kujenga timu ya 2025/26.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live