Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hans Rafael: Hakuna namba 10 kama Aziz Ki

Stephen Aziz KI VS Masandawana Aziz Ki.

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya michezo kutoka Wasafi FM, Hans Rafael amesema kuwa katika Ligi ya Tanzania, hakuna kiungo namba 10 mwenye uwezo kama kiungo wa Yanga, Stephanie Aziz Ki.

Aziz Ki ambaye ni raia wa Burkina Faso ndiye kinara wa mabao wa Ligi Kuu akiwa amefunga mabao 14 na kutoa assists 7 za mabao msimu huu.

Nyota huyo amekuwa muhimu kwenye kikosi cha Kocha Gamondi hasa kuamua matokeo hata kwenye mechi ngumu ambazo nafasi ya Yanga kushinda ni ndogo.

"Tanzania hii hakuna namba 10 kama Aziz Ki, wala hakuna namba 10 mwenye uwezo wa kupiga pasi za mwisho za mauwaji kama Aziz.

"Aziz anakupa kwenye mechi kubwa na ndogo na hiyo ndo sifa ya mchezaji mkubwa. Aziz hana uwanja wa ugenini wala wa Nyumbani," amesema Hans Rafael.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: