Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hans Rafael: Benchikha amechangia Simba kufeli msimu huu

Hans X Benchikhaaaa Hans Rafael: Benchikha amechangia Simba kufeli msimu huu

Wed, 22 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

"Nikitazama kazı ya Chasambi na Balua,naanza kupata feeling kuwa Benchikha,alichangia anguko la Simba Msimu huu.

Wakati Simba wanajiandaa na mechi ya Robo fainali ya CAF dhidi ya Al Ahly,kikosi chote kilielekea Zanzibar kujiandaa,hawa vijana (Chasambi,Karabaka na Balua) walikuwa kambini huko Zenji na walishiriki kwenye maandalizi yote.

Baada ya kurejea Dar Es Salaam,Kocha Benchikha aliwatamkia wazi vijana hao kuwa warudi nyumbani kwani hawapo kwenye mpango wake dhidi ya Al Ahly.

Ikumbukwe Simba walipoteza mechi zote mbili dhidi ya Al Ahly na Baada ya kurejea nchini wakitokea Cairo vijana hao hawakurejeshwa kwenye timu na Simba wakapoteana mbele ya Mashujaa na kutolewa kwenye mashindano ya FA.

Hii Leo amekuja Mgunda hawa vijana wamegeuka lulu,Kila siku wanaipambania timu kwa nguvu zote.

Nadhani this time Kama Simba wanakwenda kutafuta mwalimu mwingine başı lazıma atafutwe kocha sahihi mwenye Imani na vijana."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live