Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hans Pluijm asisitiza kuchukua pointi tatu mbele ya Simba

Hans Van Der Pluijm.png?fit=602%2C439&ssl=1 Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans Pluijm.

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: Nipashe

Kocha Mkuu wa Singida Big Stars, Hans Pluijm  amewataka wachezaji wa klabu yake kudhihirisha ubora wao kwa kuifunga Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa leo Novemba 9, katika Uwanja wa LITI mkoani Singida.

Kocha huyo raia wa Uholanzi amesema timu yake inataka ubingwa na raha ya kubeba ubingwa lazima kuzifunga timu kubwa kama Simba, Yanga na Azam sababu ndizo zenye malengo ya ubingwa.

“Ni mchezo mgumu sababu tunacheza na timu yenye uzoefu wa ligi lakini Singida pia ni timu kubwa yenye uwezo wa kucheza na timu yoyote Tanzania ikiwemo Simba. Wachezaji wetu wanatakiwa kuthibitisha hilo ili kuongeza heshima yao na timu,” amesema Pluijm.

Kocha huyo amesema wachezaji wake akiwemo mshambuliaji Meddie Kagere wameahidi kuleta furaha baada ya dakika 90 za mchezo huo.

Timu hizo zitakutana huku zikiwa zinalingana kwa pointi lakini Singida ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 17 sawa na Simba iliyopo nafasi ya pili zikitofautishwa na uwiano wa mabao.

Chanzo: Nipashe