Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hamisa Mobetto kuihama Simba hana mpango kabisa!

Mobeto Simba 09 03 At 11.png Hamisa Mobetto kuihama Simba hana mpango kabisa!

Wed, 31 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa wiki sasa baada ya Simba kuutangaza uzi mpya utakaotumika katika mashindano mbalimbali ya msimu ujao, mrembo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto amefunguka kwa kusema hana mpango wa kuihama klabu hiyo, tofauti na baadhi ya watu wanavyosema kutokana na kuonekana na Aziz Ki wa Yanga.

Hamisa amesema nayo baada ya watu kumuona sehemu mbalimbali akiwa na nyota huyo wa Yanga na kuzuka kwa taarifa kwamba yuko mbioni kuhamia Jangwani.

“Niseme kitu kimoja kwa mashabiki wa Simba, mie bado niko Msimbazi na wala sitegemei kuhama timu hii, na kama ikitokea kutaka kuhama nitasema tu, ila kwa sasa sina mpango na naipenda timu yangu ya Simba acha mapambano yaendelee na msimu ujao kuna matumaini makubwa timu yetu kutupa furaha,” alisema.

“Mie pia nina ndugu zangu Yanga kama mama mzazi na wengine ambao ni watu wangu wa karibu, hivyo sio kitu cha ajabu kuonekana kwangu katika matamasha au uwanjani na wanayanga,” aliongeza Hamisa.

Pi Hamisa akigusia suala la kutoonekana katika tangazo la jezi mpya za Simba za msimu ujao zilizozinduliwa hivi karibuni tofauti na alivyozoeleka, ambapo amejibu amefanya tangazo la jezi za Simba kwa miaka mingi hivyo kwa mwaka huu sio mbaya akipumzika na kuwapa nafasi wengine.

“Kwangu naona sawa tu kutofanya tangazo la jezi za Simba mwaka huu, sio mbaya kupumzika msimu huu na kuwapa nafasi wengine, ila kukosekana huko hakuna maana ndio nimehama Msimbazi. Hapana!”

Kuhusu suala la kinadada wajasiriamali Shilole na Eshe Buheti kurushiana vijembe hivi karibuni, kuhusu mashindano ya nani mpishi bora ya Dina Marios na Shilole kuibuka mshindi mwaka huu baada ya mwaka jana Eshe kushinda, kabla ya kuibuka vijembe baina ya wawili hao, Hamisa alisema: “wale ni watu wa zima wanajua wanachokifanya”.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live