Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hamasa ilikuwa juu kipindi cha Maximo - Ally Mayay

Taifa Stars AFCON.jpeg Hamasa ilikuwa juu kipindi cha Maximo - Ally Mayay

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Idara ya Michezo, Ally Mayay amesema kutotangaza kikosi cha timu ya Taifa ni kutowatendea haki wapenzi wa soka nchini.

Mayay amesema timu ya Taifa ni ya watanzania hivyo wana haki kufahamu timu yao ikitangazwa lengo kuu likiwa ni kujenga hamasa kwa mashabiki kwa ajili ya kuhamasisha wachezaji wao.

“Timu ya Taifa ni timu ya watanzania, moja kati ya habari ambayo wanahitaji kuijua ni kikosi kwa ajili ya ku-support. Mashabiki wanapenda kujua wachezaji ili kuwashabikia na kuwapa hamasa.”

“Mashabiki wengi wa soka Tanzania wamekuwa wakishabikia klabu zao za Simba na Yanga, lakini kwa Taifa Stars hamasa ilikuwa juu sana kipindi kile kocha akiwa ni Marcio Maximo.”

“Mpango ambao serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan inao juu ya timu yetu ya Taifa ni kuiunga mkono Taifa Stars na timu zote za Taifa.”

“Kwa hiyo hata mashabiki wana haki ya kupata taarifa za Taifa Stars kwa ajili ya kwenda kuiunga mkono! Nafikiri shirikisho la soka litafanyia kazi jambo hilo na kurejesha utaratibu wa kutoa taarifa mapema ili watu wajue.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live