Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hali ya majeruhi wote wa Yanga iko hivi

Yao X Auchoo Hali ya majeruhi wote wa Yanga iko hivi

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hali ya majeruhi kwa upande wa Klabu ya Yanga kutokana na ripoti ya mwisho ya daktari wa timu hiyo.

Kuna uwezekano mkubwa wachezaji wafuatao wakakosekana au kuanzia benchi kwenye mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Melodi Sundowns.

Khalid Aucho bado yupo chini ya uangalizi wa daktari hajaanza mazoezi na timu na tayari ameanza mazoezi mepesi ya msawazo wa mwili.

Kibwana Shomari ameanza mazoezi binafsi licha ya kuwa nje kwa muda mrefu.

Yao Kwasi anauguza kidonda chake mara baada ya kuchanika sehemu ya mguu mechi dhidi ya Azam FC ni 50/50.

Zouzoua Pacome bado hayupo fit kutokana na kupata enka licha ya kujumuika na timu ya taifa lake nchini Ufaransa.

Zawadi Mauya huenda akapatika kwenye mchezo ujao dhidi ya Mamelodi siku ya jumamosi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live