Kiungo wa Yanga, Khalid Aucho ameuanza mwaka vibaya baada ya kuumia akiwa mazoezini.
Aucho ambaye ni raia wa Uganda ameumia siku moja kabla ya Yanga kucheza mchezo wake wa ligi ndani ya mwaka 2023 baada ya kugongana na kipa wa timu yake.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga jioni hii, Aucho atakuwa nje kwa muda wa wiki moja kuuguza mguu wake.
Kwa muda huo Aucho anaweza kukosa mechi zisizopungua mbili zaidi za timu yake kuanzia ile ya Jumamosi Januari 21 dhidi ya Ruvu Shooting wakati akiuguza jeraha hilo.
Habari njema kwa Yanga ni kwamba kupitia majibu ya vipimo alivyofanyiwa kiungo huyo raia wa Uganda daktari wa timu hiyo Mosses Atutu amesema Aucho hajavunjika na kwamba mfupa wake umepata mshtuko na kuvimba kidogo.
"Mwanzo tulidhani ameumia sana lakini vipimo vimetuondolea hofu hiyo, vimeonyesha ni mfupa tu umevimba kidogo na tumeshaanza matibabu yake haraka," amesema Atutu.
Kwa upande wake, Aucho ameposti picha akiwa na gongo kuonyesha kuwa anaumwa kisha kuandika maneno haya;