Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hali si shwari, bundi bado anazengea Azam FC

Azam FC Muda Bado Hali si shwari, bundi bado anazengea Azam FC

Tue, 25 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hali sio shwari kwa Azam FC kwani baada ya mechi tisa tu, zikiwamo saba za Ligi Kuu Bara na mbili za Kombe la Shirikisho Afrika, mabosi wa klabu hiyo wamewapiga chini makocha wawili akiwamo Denis Lavagne aliyetua mapema mwezi uliopita.

Mfaransa huyo amesitishiwa mkataba wake akiitumikia timu hiyo kwa siku 45 tu tangu alipopangazwa Septemba 7, akiwa ni kocha wa pili msimu huu kwa Azam kutimuliwa, kwani alianza Abdulhimid Moallin aliyetimuliwa mapema msimu ulipoanza na kumpisha Lavagne.

Akiwa Azam, Lavagne aliiongoza timu katika mechi nne za ligi, ikishinda mbili dhidi ya Mbeya City 1-0 na Singida Big Stars 1-0, huku akipoteza mbili kwa Tanzania Prisons 1-0 na KMC 2-1, katika Kombe la Shirikisho aliondoshwa na Al Akhdar ya Libya kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya kuchapwa 3-0, ugenini na kushinda 2-0, nyumbani.

Mabosi wa klabu hiyo walitoa taarifa juzi ya kuachana na Lavagne na sasa timu itakuwa chini ya Kocha wa Washambuliaji, Kally Ongala akisaidiwa na nahodha Aggrey Morris anayekuwa kocha mchezaji na Mwanaspoti limepenyezewa taarifa sababu ya timua timua hiyo ya makocha ni baadhi ya viongozi wa juu kutoridhishwa na mwenendo wa timu baada ya kufanya usajili mkubwa.

Chanzo hicho ambacho hakikupenda jina lake litajwe kimeeleza mabosi hawaelewi kabisa kinachoendelea kwani wametumia pesa nyingi kwenye usajili na malengo yao ilikuwa ni kufika Makundi ya Shirikisho Afrika na kumaliza ufalme wa Simba na Yanga lakini kinachotokea ni tofauti.

Pia, taarifa zinaleleza huenda mabadiliko makubwa yakafanyika hivi karibuni kwenye uongozi wa timu hiyo na kuweka viongozi wapya. Lavagne amekuwa kocha wa tano kuachia ngazi kwenye Ligi Kuu msimu huu, baada ya Moallin, Zoran Maki aliyekuwa Simba, Joslin Sharif aliyekuwa Polisi Tanzania na Masoud Djuma aliyekuwa Dodoma Jiji bila kumsahau Juma Mgunda aliyehama Coastal Union na kutua Simba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live