Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hali ngumu ya kiuchumi yawaondoa wachezaji kutoka Tunisia

BOLI Hali ngumu ya kiuchumi yawaondoa wachezaji kutoka Tunisia

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya soka ya Ghardimaou nchini Tunisia imelazimika kusitisha shughuli zake baada ya wachezaji wake 32 kuhamia Ulaya kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu, wachezaji wake walihamia katika bara hilo jirani ndani ya miaka mitatu.

"Tumesitisha shughuli na kusimamisha mechi zetu.rais wa klabu hiyo Jamil Meftahi aliiambia AFP siku ya Jumanne, akilaumu "uhamiaji wa kinyemela".

Taifa la Tunisia limekua katika hali ngumu ya kiuchumi, hali ambayo inawalazimu raia wake wengi kukata tamaa wakichukua hatua za kutafuta maisha bora nje ya nchi.

Wachezaji hao, wenye umri wa kati ya miaka 17 na 22, waliondoka kwa kutumia bahari au Kupitia Serbia kisha wakavuka mpaka kinyume cha sheria na kuingia nchi nyingine, Meftahi alisema.

Hadi Novemba mwaka jana, raia wa Tunisia walikuwa na uwezo wa kusafiri hadi Serbia bila visa, na kuwapa maelfu ya watu njia mbadala ya kuvuka kwa mashua katika Bahari ya Mediterranian ambayo ni njia mbaya zaidi ya uhamiaji duniani.

Meftahi amelaumu ukosefu wa uwezo wa kifedha kama sababu ya wachezaji hao kuondoka kwao. "Hatuwezi kumudu vifaa, jezi au viatu, na wachezaji hawalipwi," alisema Meftahi.

Sehemu za pwani ya Tunisia ziko ndani ya maili 90 (kilomita 150) kutoka kisiwa cha Italia cha Lampedusa, na maelfu ya watu Watunisia na raia wa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara wamejaribu kuvuka tayari mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live