Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hali Tete Morocco, Chama Aahidi Kurejea Simba

John Bocco Meddie Kagere And Clatous Chama Of Simba?fit=700%2C423&ssl=1 Chama

Wed, 6 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

ALIYEKUWA nyota wa Klabu ya Simba, Clatous Chota Chama ameahidi kurejea katika kikosi cha Simba baada ya nyota huyo kutoa ahadi hiyo kwa Jonas Gerard Mkude kupitia mtandao wa Instagram.

Clatous Chama aliachana na Simba baada ya msimu wa 2020/21 kutamatika ambapo nyota huyo alijiunga na Klabu ya RS Berkane ya nchini Morocco tayari kwa kuitumikia klabu hiyo kuanzia msimu wa 2021/22.

Huku akifanikiwa kuichezea klabu hiyo katika jumla ya michezo mitatu bila kutoa pasi ya bao au hata kufanikiwa kuipatia bao klabu hiyo. Hii ni kwa mujibu wa mtandao wa transfermarkt.com katika michezo ya Ligi Kuu ya nchini Morocco.

Hali hii imemfanya nyota huyo kuanza kuikumbuka Klabu yake ya zamani, Simba Sports Club hii ni baada ya nyota huyo kuweza kufichua matamanio yake ya kurejea tena nchini Tanzania. Huku akiweka wazi matamanio hayo kwa nyota wa klabu ya Simba, Jonas Mkude.

Ambapo Oktoba 3, 2021 Jonas Mkude aliweka chapisho katika mtandao wa Instagram huku akiambatanisha picha yake. Lakini katika hali ya kushangaza aliyekuwa nyota wa klabu ya Simba, Chama alijibu chapisho hilo kwa kusema kuwa anakuja.

Lakini baada ya jibu la Clatous Chama, nyota wa klabu ya Simba, Jonas Mkude alimjibu kwa kumwambia kuwa amemkumbuka sana huku akionesha alama ya kucheka mwanzoni mwa jibu lake katika chapisho hilo.

Hii inatoa ishara kuwa Clatous Chama kuna muda anakumbuka maisha ambayo ameyaishi na nyota wenzake katika klabu ya Simba. Hali ambayo imemfanya atamani kujumuika nao tena kwa mara nyingine japokuwa tayari amekwisha kuanza majukumu yake katika klabu mpya.

Pia utawala ambao nyota huyo alikuwa ameshafanikiwa kuuweka katika klabu ya Simba hasa katika mioyo ya washabiki, wanachama wa klabu ya Simba na wapenzi wa soka nchini Tanzania unamfanya akumbuke mengi ikiwemo kumbukumbu ambazo ameziweka akiwa katika ardhi ya Tanzania.

Hivyo basi kutokana na changamoto mpya ambazo amekuwa akikutana nazo katika klabu yake mpya ya RS Berkane, Chama ameanza kutamani ulimwengu ambao ameuishi katika ardhi ya Tanzania akiwa na nyota wenzake kama Jonas Mkude.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live