Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna wa kumzidi Pacome kwa sasa Bongo - Jemedari

Hakuna Wa Kumzidi Pacome Kwa Sasa Bongo   Jemedari.jpeg Hakuna wa kumzidi Pacome kwa sasa Bongo - Jemedari

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Jemedari Said ameshusha ujumbe kwenye ukurasa wake wa Instagram akieleza kuwa kiongo mshambuliaji wa Yanga pacome Zouzoua ndiye mchezaji mwenye thamani zaidi katika Ligi Kuu ya NBC.

"Mpaka sasa hakuna mchezaji kwenye Ligi Kuu bara ana performance kumzidi au sawa na PACOME ZOUZOUA wa Yanga SC ambaye ni raia wa Ivory Coast.

"Ukiachana na takwimu zozote unazozijua kumhusu lakini uwezo wake wa kucheza soka kama ‘Sanaa ya maonyesho’ ni mkubwa na unaotoa furaha na burudani hatakama wewe si Gongowazi.

Amefanikiwa kuulazimisha mpira kutii mambo mengi yanayoanzia kichwani na kuhitimishwa kwenye miguu yake. Anajua kupasia, kukokota na inapobidi kufunga mabao hufunga.

"Mabao 3 Champions League na 6 kwenye ligi kuu ni ushahidi wa namna kiungo wa pembeni anavyoweza kuifanya kazi yake ya pili kwa ubora mkubwa. Ushindi wa bao 4 mbele ya CR BELOUZIDAD hakufunga lakini mchango wake ulikuwa mkubwa, PACOME DAY was perfect idea."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live