Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna uhakika wa namba KMC, kila eneo lina mtu

Awesu Awesu Awesu Awesu

Thu, 9 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watoza ushuru wa Manispaa ya kinondoni KMC, msimu ujao wamepanga kufanya vyema zaidi kama ilivyokuwa misimu miwili iliyopita walipofanya vyema zaidi katika ligi kuu Tanzania Bara.

Ili kuendana na dhamira yao KMC wamefanya usajili katika maeneo mbali mbali ili kuhakikisha wanajikamilisha kila idara ya kikosi chao.

kutokana na Usajili huo wamejikuta wakiwa na ushindani mkubwa wa namba ndani ya kikosi chao.

Kocha Msaidizi wa KMC, Habibu Kondo amesema “Nafarijika kuona kila mchezaji wangu anapambana kwa nguvu zote ili kupata nafasi ya kucheza, hii inaonyesha msimu ujao tutafanya vizuri zaidi tofauti na msimu uliomalizika,” amesema.

“Ukiangalia KMC imetimia kuanzia idara ya ulinzi hadi ushambuliaji, kila nafasi ina watu wa maana ambao wana uzoefu na Ligi Kuu Bara,” amesema.

Katika hatua nyingine Kondo alisema wachezaji waliosajiliwa ni pendekezo lake hivyo hatokuwa na kisingizio chochote wakati ligi itakapoanza.

“Nawashukuru viongozi wangu kwa kuifanyia kazi vyema ripoti yangu kwani wameniletea wachezaji ambao niliwapendekeza mwenyewe,” amesema.

Amesisitiza anachokifanya kwa wachezaji wake ni kutengeneza utimamu wa mwili kabla ya kuanza mikakati ya kutafuta mechi za kirafiki.

Wachezaji wapya waliosajiliwa na kikosi hicho ni golikipa Farouk Shikhalo aliyetokea Yanga baada ya mkataba wake kumalizika huku wengine wakiwa ni Hassan Kessy, Miraj Athumani, Awesu Awesu, Iddi Kipagwile na Nickson Kibabage.

KMC pia imemrejesha aliyekuwa mshambuliaji wake za zamani Charles Ilamfia kwa mkopo wa Mwaka mmoja baada ya kuwa na wakati mgumu Simba.

Klabu ya KMC iliweka kambi yake kule mkoani Morogoro kwa muda wa wiki mbili ili kujiandaa na msimu mpya wa Ligi kuu Bara 2012/2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live