Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna tofauti ya Pacome na Fei Toto - mchambuzi

Fei Toto X Pacome Hakuna tofauti ya Pacome na Fei Toto - mchambuzi

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka kituo cha runinga cha TV3, Alex Ngereza amesema kuwa mambo anayoyafanya kiungo mshambuliaji wa Yanga, Pacome Zouzoua yameshafanywa mara nyingi na aliyekuwa kiungo wa timu hiyo ambaye kwa sasa yupo Azam FC, Feisal Salum 'Fei Toto'.

Kauli hiyo ya Ngereza inakuja ikiwa ni siku chache baada ya mashabiki kummwagia sifa mitandaoni kingo huyo raia wa Ivory Coast kutokana na mahiri wake kwenye soka jambo ambalo kwa kushirkiana na wachezaji wake ameisaidia Yanga kutinga robo fainali ya CAFCL kwa kuifunga CR Belouizdad bao 4-0 weekend iliyopita.

"Sijaona tofauti kati ya Feisal Salum na Pacome Zouzoua. Hivi ambavyo Pacome anavifanya kwenye mpira wetu Feisal Salum kavifanya sana na anaendelea kuvifanya. Ila kwa sababu ni Mtanzania na Watanzania wanapenda sana wageni, Pacome atapata sifa nyingi sana kuliko Feisal Salum," amesema Mchambuzi Alex Ngereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live