Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

'Hakuna shida yoyote kisheria Yanga kutumia logo ya Simba'

'Hakuna Shida Yoyote Kisheria Yanga Kutumia Logo Ya Simba' 'Hakuna shida yoyote kisheria Yanga kutumia logo ya Simba'

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakili kutoka ofisi ya mawakili ya Mzizima Advocates, amesema haoni tatizo lolote Yanga kutumia logo ya Simba kwenye bango lao.

Hiyo imekuja kufuatia Yanga kuweka bango kubwa barabarani la matokeo yao waliyomfunga Simba hivi karibuni 5-1.

“Hili suala la Yanga kuweka mabango hata mimi nimeliona, kisheria sioni madai yoyote ambayo Simba anaweza kuwa nayo dhidi ya Yanga, Yanga wamechukua video ambayo imetengenezwa na Azam TV.

“Mwenye umiliki wa hayo maudhui ni Azam TV, TFF na Bodi ya ligi wameuza maudhui yote kwa Azam TV na wao wana exclusive right.

“Ukija kwenye uwanda huo Yanga wametumia maudhui ya Azam TV, mtu ambaye ana ukaribu na hili ambaye angeweza kudai chochote ni Azam TV kama Yanga wameyatumia bila idhini,” alisema wakili huyo kutoka ofisi ya mawakili ya Mzizima Advocates.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live