Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna sababu ya kumlalamikia Mo Dewji

Mangungu Mo Dewji Hakuna sababu ya kumlalamikia Mo Dewji

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa Klabu ya Simba ina viongozi wake ukimwondoa mwekejazi MO hivyo ni wajibu wa viongozi hao kutolea ufafanuzi suala la uwekezaji wa tajiri huyo.

Inasikitisha kuona baadhi ya mashabiki wanasema MO hatoi pesa Wakati timu inamudu gharama zote ikiwemo mishahara za wachezaji pamoja na kambi za pre season nyingi.

Ikiwa MO hatoi pesa ni jukumu la uongozi wa Simba kusema pesa hizo za kuitesha timu wanazitoa wapi?

MO mara kadhaa amekuwa akilalamika kula hasara kwenye uwekezaji wake Simba..ni sawa mana ikiwa siyo sawa je uongozi wa Simba chini ya Mangungu umelikanusha hilo?

Hivyo kama MO ataondoka Simba basi jua itahangaika sana kwa kuyumba kiuchumi. Ni ushabiki tu usio na tija wala kutaka kuchallenge akili kutaka kujua sababu.

Mashabiki wa Simba wanaohitaji MO aondoke ndio hao watakaotaka MO arudi baada ya kuondoka Simba Sc.

Wanasimba kila club duniani inapitia nyakati ngumu. Man U, Barcelona, Chelsea, Bayern Munich zote zinapitia hali ya sintofahamu, vumilieni na tatueni changamoto kwa upande wenu na siyo kwa mwekezaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live