Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna mwamuzi anayeidai posho - Bodi ya Ligi

Hakuna Mwamuzi Anayeidai Posho   Bodi Ya Ligi Hakuna mwamuzi anayeidai posho - Bodi ya Ligi

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), Almas Kasongo amesema leo Agosti 15, 2023 wanakwenda kufungua pazia la Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023-24 kukiwa hakuna mwamuzi hata mmoja anayedai posho yake.

Akizungumza na Wasafi FM mapema hii leo, Kasongo amesema lengo lao ni kuona changamoto zote zilizobainika kwenye msimu uliopita, wamezifanyia kazi ili kuzidi kuboresha ili msimu huu uwe bora zaidi ya uliopita.

"Waamuzi wamefanya mazoezi ya utimamu wa mwili, wamekaa darasani kujifunza sheria 17 za mpira na wametuhakikishia kwamba wataondoa makosa kabisa yaliyokuwa yakijitokeza," alisema Kasongo.

Ligi hiyo inaanza leo kwa michezo mitatu ya raundi ya kwanza ambapo Ihefu watawakaribisha Geita Gold, Namungo atakipiga na JKT Tanzania huku Dodoma Jiji akiwakaribisha Coastal Union.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live