Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna mpango wa kumfukuza Solkjaer licha ya kupoteza dhidi ya City

Skysports Ole Gunnar Solskjaer 5576311 Kocha wa Man U, Ole Gunner Solkjaer

Mon, 8 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ushindi dhidi ya Spurs na sare dhidi ya Atalanta ugenini, ambao umewaweka katika uongozi wa kundi Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki iliyopita, umeonekana kutuliza hali ya mambo kwa Meneja wa Man United, Ole Gunner Solskjaer aliekuwa anatizamiwa kuondolewa ndani ya kikosi hicho.

Hakuna dalili kutoka ndani ya uongozi wa Klabu zinazoonesha Solskjaer atapoteza kibarua na zaidi inatarajiwa ataonekana akiwa katika majukumu yake watakapovaana na Watford baada ya Mapumziko ya Timu za Taifa.

Tetesi za kutala Ole afukuzwe zilikuja baada ya kupokea kichapo cha goli 5-0 wiki mbili zilizopita, lakini ushindi dhidi ya Spurs ugenini, sare dhidi ya Atalanta na kuwafanya waongoze kundi lao michuano ya Ulaya umeonekana kutuliza hali ya mambo ndani ya Klabu.

Akizungumza baada ya ushindi wa city, mchambuzi wa Kituo cha Soka cha Sky Sports na gwiji wa zamani wa Man United Garry Neville, amesema maamuzi yoyote kwa sasa hayawezi kuchukuliwa mpaka baada ya kuondoka kwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo Edwoodward mwishoni mwa mwaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live