Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna mapumziko Mtibwa, Omog anataka kazi

Pjimage (27) Kocha Omog hajafurahishwa na matokeo ya Mtibwa Sugar

Tue, 5 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mpya wa Mtibwa Sugar, Joseph Omog ameamua kutowaruhusu wachezaji wake kwenda kwenye mapumziko kipindi hiki ambacho ligi imesimama kupisha mechi za kimataifa za kalenda ya FIFA.

Wachezaji wa Mtibwa wameendelea kufanya mazoezi kwa saa nane kwa siku [saa nne asubuhi na saa nne jioni].

Mtibwa Sugar ilipoteza mchezo wake wa kwanza kwenye ligi [Mtibwa Sugar 0-1 Mbeya Kwanza] halafu ikatoka suluhu kwenye mchezo wa pili [Mtibwa Sugar 0-0 Tanzania Prisons]. Kwa takribani misimu miwili iliyopita Mtibwa Sugar imenusurika kushuka daraja na kujikuta ikicheza michezo ya mtoano (Play off).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live