Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna mapumziko Dodoma Jiji

WhatsApp Image 2023 11 09 At 14.jpeg Hakuna mapumziko Dodoma Jiji

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: Dar24

Benchi la ufundi la Dodoma Jiji chini ya Melis Medo na msaidizi wake Kassim Liogope limeamua kutowapa mapumziko wachezaji wake katika siku zaidi ya 10 ambazo Ligi Kuu Tanzania Bara itasimama kupisha timu ya taifa, ili kuwaimarisha zaidi.

Kocha Liogope amesema msimu huu wanataka kufanya vizuri na bado alama walizonazo hazitoshelezi hivyo wanaamini muda huo wa siku 10 utatosha kuwafanya wawe bora zaidi.

Tumekusanya alama nyingi kwa wakati mmoja kutokana na mikakati tuliyojiwekea tukiwa Misungwi kujiandaa na Geita hadi sasa, tumeamua kama makocha tusiende kupumzika bali tumebaki Dodoma na baada ya siku mbili hizi, timu irudi kambini kujiandaa na mechi zijazo,” amesema Liogope.

Katika mechi nne zilizopita za Ligi Kuu, Dodoma Jiji imekusanya, idadi ya alama 10 ambazo zimeifanya isogee hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi ikiwa na alama 15.

Chanzo: Dar24
Related Articles: