Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna kiingilio mechi ya Twiga Stars

TWIGA STARS,TZ Timu ya Taifa ya Wanawake "Twiga Stars"

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa taarifa ya kuruhusiwa kwa mashabiki katika mchezo wa kufuzu michuano ya Afcon kati ya Twiga Stars na Namibia utakaopigwa kwenye uwanja wa Mkapa Jijini Dar es salaam.

Katika taarifa hiyo TFF ilifafanua kwamba wapokea ruhusa hiyo ya kuingiza mshabiki kutoka Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) saa 7:25 mchana.

Aidha kutokana na muda mfupi uliopo hadi kufikia mchezo huo kuanza saa 10:00 TFF wameruhusu mashabiki kuingia bure.

Baada ya mchezo huo Twiga itakuwa na kibarua cha mchezo wa marudiano kule Namibia Oktoba 23 na ikifanikiwa kupita itakutana na mshindi kati ya Malawi na Zambia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live