Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakimu: Huyo Mayele alinitoa jasho

Hakim Pic Hakimu: Huyo Mayele alinitoa jasho

Mon, 3 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kipa wa Ruvu Shooting, Isihaka Hakimu, mwenye historia ya pekee msimu uliomaliza mwezi uliopita kwa kutokufungwa na straika hatari wa Ligi Kuu, Fiston Mayele akiungana na makipa wachache ambao hawakulizwa na nyota huyo wa Yanga kutoka DR Congo.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 25 anaidakia Ruvu Shooting na alikuwa uwanjani kwenye mechi ya mwisho baiona ya timu hiyo na Yanga na Mayele kushindwa kutetema, licha ya timu yake kupoteza mchezo mbele ya mabingwa hao wa kihistoria wa Tanzania.

Ruvu ni kati ya timu ambazo hazikufungwa na Mayele kwenye Ligi Kuu ikiwamo Simba ambao kwa bahati mbaya ilishakutana na straika huyo mara mbili mfululizo kwenye Ngao ya Jamii na kuwapiga nje ndani.

Katika mahojiano yake na Mwanaspoti, kipa huyo aliyezaliwa na kukulia Unguja, visiwani Zanzibar na kuanza soka mtaani kabla ya kuibukia Tanzania Bara aliposajiliwa katika dirisha dogo amefunguka mambo mengi aliyopitia kwenye safari yake ya soka na kukiri Mayele ni bonge la straika anayetisha.

MTAANI BALAA

Kipa huyo anasema alianza kucheza soka la ushindani kwenye timu ya New Boy Academy iliyopo Zanzibar akiwa na timu hiyo alipata nafasi ya kupandishwa timu ya wakubwa na kuituimikia kwa kipindi cha msimu mmoja kabla ya kuingia Pajes ya wakubwa na kuwa nao kwa msimu mmoja.

Baada ya hapo aliisajiliwa Mlandege Fc iliyokuwa daraja la kwanza akti huo na nikafanikiwa kuipandisha kwenda Ligi Kuu na tuluicheza kwa mafanikio makubwa sana.

Anasema kuwa walipoingia Ligi Kuu laiifanikisha timu yake kuingia nafasi ya nne na alitumika mpaka walipokuwa Mabingwa na kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2022\2023 walitoka hatua za mwanzoni kabisa.

"Nilicheza Ligi ya Zanzibari kwa mafanikio makubwa kwani haja yangu ilikuwa ni kuwaonyesha walionidharau na walionipa nafasi kuwa naweza," alisema Isihaka.

MTONYO BARA HATARI

Kipa huyo anasema utofauti wa Ligi ya Zanzibar na Bara kwa upande wake ni mkubwa kwani kwa anaiona fursa ya hela kuwa pana zaidi Bara.

Anasema kuwa wakati anacheza kule hakuweza kuwa na kipato kizuri kama alipo sasa ijapokuwa sio kikubwa ila huku kuna nafasi nzuri ya kupata jina endapo utafanya viuzuri.

"Mpango wangu wa kwanza ulikuwa kuchezsa Bra kwani Ligi yake inampa mchezaji fursa yua kujulikana na kupata pesaa nzuri kutokana na ushindani mkubwa wa soka uliopo," alisema Isihaka.

SIRI IKO HAPA Isihaka nan sema wakati anasajiliwa alikuwa akicheza nadfasi ya tatui ila aliamua kupambana na kuonyesha kile alichonacho kwa ukubwa na kuingia kikosi cha kwanza.

Anasema kuwa wakati alipoanza alijianda kwani ugumu ulikuwepo kwani tayari eneo alilosajiliwa aliwakuta watu na hii ndio kazi yao hivyo ukiingia unakuwa kama adui na sio rafiki.

"Niliingia kwa mara ya kwanza kwenye mechi na nikajua hapa ndio nafasi ya kuonyesha kile mnilichona ili nipate nafasi zaidi kwani kwangu ilikuwa ndoto kuanza kikosi cha kwanza hivyo siri yangu kubwa ni kutumia muda wote niliopewa vizuri,

"Mechi yangu ya kwanza ilikuwa FA dhidi ya Ndanda Fc na Ligi Kuu nilipata mafanuikio makubwa kwa kupatta Clean Shirt tano dhidi ya Coast Union,Mtibwa na Police," alisema Isihaka.

MALENGO MAZITO

Kipa huyo anasema amekuwa akiichezea nafasi hiyo tangu aujue mchezo huu hivyo mpango wake ni kuwa bora zaidi ili aweze kupata fursa za kucheza ndani na nje ya Nchi.

Anasema hakuna anachokitaka zaidi ya kukua na kujifunza kwa waliobora zaidi ilikuongeza ujuzi wake kwani bado anasafri ndefu ya kuelekea kule anako kwenda.

"Najifunza kwa Makipa walioendelea kwa lengo la kuwa bora kwani ushindani ni mkubwa bila kuwa na utulivu uwanjani na kuangalia nini wengine wanafanya ni ngumu kufanikiwa.

"Timu ambazo natamani kuchezea Ligi Kuu ni Simba,Yanga,Azam na Singida hizi ni timu bora kwa sasa na mimi kama mchezaji bora natamani kuzitumika," alisema Kipa Isihaka.

MAYELE HATARI

Isihaka anasema kwenye Ligi ya Bra amecheza na wachezaji wengi wa timu tofauti lakini mshambuliaji wa timu ya Yanga ndie aliewahi kumpa changamoto zaidi uwanjani.

Anasema hakuweza kuruhusu mashambulizi yake matano katika mechi dhidi ya Yanga hali iliyomfanya awe makini zaidi pindi mshambuliajihuyo alipokuwa na mpira.

"Niliokoa mipira mitano ya Mayele katika mechi moja na kutengeneza historia ya kutokufungwa na mshambuliaji huyo hali ambayo sio rahisi kwake kwani mshambuliuaji hatrari sana kwenmye Ligi hii," alisema Isiaka.

NJE NA SOKA

Isihaka anasema nje na soka huwa anapendelea zaidi kufanya shughuli za ujenzi na uvuvi kwani ndio shughuli anazopenda zaidi kuzifanya wakati wa mapumziko yake. Anasema kuwa kuvua kwa watu wa unguja ni jambo la kawaida kwani ndio kazi unayofanywqa na watu wengi huko na kuwaingizia kipato.

"Uvuvi na ujenzi ndio kazi ninazofanya nje na uwanja na huwa nazipenda kwani nimekuwa na kuona zikifanyika hivyo nina ujuzi nazo kwani asili ya eneo nililozaliwa shughuli hizi zinafanyuka sana," alisema Isihaka.

KIJIJI KIZIMA

Isihaka anasema amekulia kijiji cha Paje na yeye ndie mchezaji aliyekuwa anachezea Ligi Kuu hivyo heshima na mwamko wa watu wengi ni mkubwa pindi anapokuwa akifanya vizuri.

Anasema familia yake kwa ujumla ni mashabiki wakubwa wa mpira na kupelekea kucheza kwa juhudi tangu utotoni kwani watu wengi wanamuona kama mfano wa kuigwa.

"Familia, Kijiji na Mkoa wa Unguja kwa ujumla wanamuonyesha upendo kama mchezaji ninaewawakilisha ndio maana hatamani kuwaangusha kabisa." anasema Isihaka ambaye anawakubali Aishi Manula, Diarra, Feisal Salum, Fiston Mayele na Henock Inonga.

ROHO MBAYA

Anasema amewahi kukutana na watu walimkatisha tamaa na kumwambia hakuna anachokifahamu kwenye soka bora akafanye mambo mengine na sio soka.

Isihaka aliendelea kusema wakati hayo yanatokea tayari alikuwa na picha ya wapi anataka kwenda hivyo hakukta tamaa wala kurudi nyuma kwa mambo kama hayo.

"Ukiwa na kipaji kikubwa tegemea kukatishwa tamaa kwani hakuna jambo liunaweza kuua ndoto za mtu yoyote kama akiruhusu kuishi maisha ya maneno ya watu."

MAJONZI YANGU

Jambo pekee ambalo limenikata maini katika soka ni timu yangu kushuka daraja na wakati huo nilipojiunga nayo malengo yangu ya kucheza Ligi Kuu yalianza kukamilika.

Anasema hawezi kutoa taarifa kuwa anakwenda timu gani kwani hajawasiliana na kikosi chochote hivyo yeye nin mchezaji wa Ruvu Shooting bado.

"Bado tuna nafasai ya kufanya vizuri na kuoanda tena matokeo ya namna hii yanaweza yasivutie sana ila yanafundisha kitu hasa kwa uongozi na pia wachezaji."

Isihaka anasema hatasahi michezo migumu zaid kwake ambapo alifungwa mabo mengi zaidi na kutoka uwanjani akiwa amechoka na maumivu makali moyoni.

Anaendelea akisema alifungwa mechi ya kirafiki akiwa na Mlandege na Yanga na kupigwa mabao matano na mashindano ya Club Bingwa Afrika dhidi ya Tunisia na klupigwa idsadi hiyo hiyo.

"Ilikuwa michezo nil;iyokutana na timu bora zaidi kwani kwangu haikuwa rahisi kucheza nao kutokana na wachezaji wenzangu kuzidiwa nguvu na vikosi hivyo vilivyona uzofu wa kuwasoma wapinzani kuliko sisi."

WASHIKAJI

Nina marafiki ambao wamekuwa kama familia kwangu ijapokuwa bado ni mgeni ila wapo ambao wamekuwa karibu yangu mpaka sasa.

Kwa upande wa Ruvu ni Haruna Chanongo na Albakasim na nje ya kikosi chetu ni Kipa wa Geita Gold Yussuf Abdi hawa wachwzaji jnje na kazi wamekuwa familia kwangu," alisema Isihaka.

Chanzo: Mwanaspoti