Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haji Manara arudisha kombora Kamati ya Rufaa

MANARA 35454657 1 Haji Manara

Thu, 15 Sep 2022 Chanzo: dar24.com

Baada ya kutangaza kupunguziwa adhabu ya Faini kutoka Milioni 20 hadi Milioni 10 lakini anaendelea na adhabu ya kifungo cha miaka miwili cha kutojihusisha na Soka, aliyekua Msemaji wa Young Africans Haji Manara ameibuka na kuonesha kupuuzwa kilichotangazwa na Kamati ya Rufaa ya TFF.

Manara ameweka andiko la kupuuzia maamuzi ya Kamati ya Rufaa ya TFF katika Kurasa zake za Mitandao ya Kijamii, miongoni mwa maelezo yake aliyoandika yanayoonekana kuwapuuza Kamati hiyo ni: Alhamdulillah

Yes, yaliyotangazwa jana na Wafalme juu yangu, ni sehemu ya Changamoto zetu za kidunia na niliyatarajia Pasi na Shaka.

Ndugu zangu, jamaa, marafiki na Wananchi wenzangu msifadhaike hata tone na hizi hukumu dhidi yangu,,Haki haijawahi kushindwa milele, is the matter of time.

Tuendelee kuwa na Subira Kwa Mungu ,Mungu aliye Mkuu na anaetujua sote waja wake na tunayoyatenda kwa dhahiri na kwa siri.

Chanzo: dar24.com