Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haji Manara aonekana kwenye kambi ya Simba

IMG 20220812 WA0017 Manara Haji Manara

Fri, 12 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Muhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Haji Sunday Manara, leo Ijumaa, Agosti 12, 2022 ameonekana City Lounge Hotel ambako inasemekana Klabu ya Simba imeweka kambi kwa ajili ya mechi ya kesho ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga.

Haijafahamika mara moja kuhusu Manara ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa miaka miwili na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), alifuaata nini hapo ilihali vilabu hivyo viwili vya Kariakoo ni mahasimu wa enzi na enzi

Picha zilizopigwa katika eneo hilo na kusambaa mitandaoni leo zinamuonesha Manara akiwa eneo la mapokezi la hoteli hiyo.

Ikumbukwe kuwa, mwishoni mwa msimu wa ligi kuu mwaka 2020/21, Manara akiwa mhamasishaji wa Simba alituhumiwa na uongozi wa klabu yake kuwa anafanya mawasiliano na viongozi wa Yanga na kuihujumu klabu yake ya Simba (wakati huo), sakata hilo ndilo lilimng'oa Manara katika klabu ya Simba na kuhamia Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live