Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haji Manara: Wanaosema bao la kuotea waende vituo vya polisi kutoa maelezo

94582 Pic+manara Haji Manara: Wanaosema bao la kuotea waende vituo vya polisi kutoa maelezo

Thu, 6 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Afisa Habari wa Simba, Haji Manara amewataka wale wanaolalamika Simba imefunga bao la kuotea, waende vituo vya polisi kwa ajili ya kutoa maelezo.

Kauli hiyo ya Manara imekuja baada ya Simba kufunga bao la kusawazisha alilofunga John Bocco akiwa katika eneo la kuotea katika ushindi wao wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania.

Akizungumzia tukio hio Manara alisema wale wanaolalamika Simba imefunga bao la kuotea, wanatakiwa kwenda kwenye vituo vya polisi kwa ajili ya kutoa maelezo.

“Wanatakiwa kwenda vituo vya polisi bila ya wasisahau kubeba vitambulisho vya Nida.”

Bocco alifunga bao hilo katika dakika 57, akipokea pasi ya Clatous Chama akiwa katika eneo la kuotea na kutuliza mpira kabla ya kupiga shuti lililojaa wavuni.

Mwamuzi wa kati Hance Mabena alionyesha mpira kupelekwa kati kuashilia bao, lakini mwamuzi msaidizi Joseph Masija kutoka Mwanza yeye alisimama akiwa hajarudi kati kuonyesha kwamba goli limefungwa.

Pia Soma

Advertisement
Hali hiyo iliwafanya wachezaji wa Polisi Tanzania kubaki wakishangaa kuona maluweluwe yaliyokuwa yamefanywa na Mwamuzi Mabena.

Kipa wa Polisi Tanzania, Mohamed Yusuf alionekana kumfuata mwamuzi msaidizi, Joseph Masija na kuzungumza naye kwa ukali wakati huo huo mwamuzi wa kati Mabena alimfuata na kumpa kadi ya njano.

Tukio la bao hilo ni muendelezo wa malalamiko ya wadau wa soka kwa waamuzi kushindwa kutafsiri vizuri sheria ya kuotea inayoonekana kuwapa faida zaidi Simba katika siku za karibuni.

Mshambuliaji Ajibu akiingia akitokea benchi alifunga bao la pili la Simba katika dakika 90+5 akiunganisha pasi Meddie Kagere huku Sixtus Sabilo akifunga bao la kufutia machozi kwa Polisi Tanzania katika dakika 22.

Wadau hao wa soka waliwalalamikia uamuzi yaliyotolewa na baadhi ya waamuzi waliochezesha mechi hiyo, hawakwenda sawa na sheria 17 za mchezo.

Waamuzi hao wa kati alikuwa, Hance Mabena kutoka Tanga na wasaidizi wake, Anord Bugado wa Tanga, Joseph Masija wa Mwanza na wa akiba alikuwa, Hamis Changwalu wa Dar es Salaam.

Chanzo: mwananchi.co.tz