Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haji Manara: Nimekaribia kufunguliwa

Manara Sanukeni.jpeg Haji Manara.

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amefunguka kuwa adhabu yake aliyopewa na Shirikisho la Soka Tanzania chini ya Kamati ya Maadili kutokana na makosa ya kinidhamu, ikarabibia kufika ukingoni.

Julai 2022, Manara alipigwa bani ya kutojihusisha masuala ya soka kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya Tsh milioni 10.

"Trehe 20 July Inshaallah adhabu yangu itakuwa imeisha kwa mujibu wa Judgement yao, ni chini ya mwezi mmoja toka tarehe ya leo.

"Nina hamu kubwa ya kuja kukamilisha project flani kwa ushirikiano na wenzangu ndani ya Young Africans walau kwa mwka mmoja au ziada kidogo.

"Lakini nime-miss mno uwepo wangu kwenye Siku ya Mwananchi, kiufupi mimi mwenyewe nimeji-miss kutokuwepo kwangu kwenye Holiday yetu."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live