Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haikuwa rahisi kwa Kane

Sanamu Ya Harry Kane Imehifadhiwa Kwa Miaka Mingi Harry Kane

Sat, 2 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Unapotazma maisha ya nyota wa Bayern Munich, Harry Kane, ni rahisi kufikiri ana kipaji ambacho hakuwahi kukumbana na changamoto yoyote.Kane atakuambia hiyo sio kweli kile anachokifanya kimejengwa na bidii.

“Nilipokuwa mdogo, nilitolewa kutoka klabu moja na kwenda nyingine, na kisha nilipokuwa kijana, 17, 18, nikitoka kwa mkopo, nikiishi peke yangu kwa mara ya kwanza, mambo hayakuwa sawa, ndipo ninapoangalia nyuma,” Kane aliambia BBC Sport.

“Ilinibidi kuonyesha zaidi, kujiamini sana, ustahimilivu mwingi katika nyakati hizo. Nilikuwa na bahati ya kuwa na familia nzuri karibu nami, rafiki wa kike mzuri wakati huo ambaye ni mke wangu sasa, hivyo niliweza kushinda nyakati ngumu, niliekekeza fikra na mawazo yangu kwenye kiwanja cha mazoezi hatimaye mambo yakajipa na kuwa mchezaji niliye kwa sasa.”

Kane anajua hadithi yake ni ya kipekee, pia anahisi ni muhimu kwa wengine wanaoweza kuwa katika hali hiyo kuelewa jinsi umakini na uvumilivu ni muhimu kwa safari ya mwanasoka.

Chanzo: Mwanaspoti