Mchambuzi wa masuala ya michezo, Alex Ngereza amedai kuwa mshambuliaji mpya wa Yanga, Hafiz Konkoni raia wa Ghana anaweza asifanye vizuri ndani ya klabu hiyo kutokana na historia ya Ligi Kuu ya Tanzania kushindwa kuwa rafiki kwa washambuliaji ambao wanatoka Ghana.
Ngereza ameongeza pia kuwa, Konkoni (23) angekuwa na uwezo basi angesalia Ulaya alikokuwa akicheza badala ya kurejea nyumbani Afrika ambako changamoto ni nyingi kuliko Ulaya.
"Nina waswas Hafiz konkon anaweza asifanye vizuri kwenye Klabu ya Yanga hasa baada ya kushindwa kufanya vizuri huko Ulaya sehemu ambayo ina kila kitu tena ameondoka akiwa na umri mdogo sana kama angekuwa mshambuliaji mzuri asingerudi nyumbani.
"Na Hapa kwetu Tanzania changamoto ni nyingi kwanzia kwa viongozi, mashabiki,viwanja na ni sehemu ambayo washambuliaji wengi kutoka Ghana wameshindwa kufanya vizuri kutokana na ugumu wa ligi yetu," amesema Ngereza.
Yanga imemsajili Konkoni kutoka Bechem United ya Ghana kwa kandarasi ya miaka miwili kuziba pengo la Mkongomani Fiston Mayele anayetajwa kujiunga na Pyramid ya Misri baada ya msimu uliopita kumaliza na mafanikio ya kuwa mfungaji bora Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika.
Mrithi huyo wa Mayele msimu uliopita katika ligi ya Ghana alifanikiwa kufunga mabao 15 kwenye mechi 26 na kutoa assist 3 akimaliza nafasi ya pili. Kabla ya Konkoni kusajiliwa na Yanga alikuwa akihusishwa klabu ya Al Hilal ya Sudan.
MRAKIBU mwandamizi mstaafu wa Jeshi la Polisi, Masuke Mponeja amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kujitambulisha kwa jina la mtu mwingine aliyetajwa katika cheti cha kumaliza kidato cha sita. - Masuke alifikishwa mahakamani hapo juzi na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Happy Mwakanyamale mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Ferdnadri Kiwonde. - Akisoma hati ya mashitaka, Mwakanyamale alidai kuwa kati ya Juni 1984 na Septemba 8, 1986 katika eneo la Ukonga na Ofisi za Jeshi la Polisi zilizopo ndani ya Wilaya ya Ilala aliwasilisha cheti cha Kidato cha Sita kilichotolewa na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kwa Geni Vitus Dudu chenye namba S.147/511 na kujifanya ni yeye huku akijua si kweli na ni kinyume cha sheria. - Mwakanyamale amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kusoma hoja za awali. Masuke alikana kuhusika na mashitaka hayo. - Mshitakiwa ameiomba mahakama kumpatia dhamana kwa kuwa ana matatizo ya shinikizo la damu na sukari na kutumia vyakula maalumu. - Pia ameiomba mahakama hiyo kupanga kesi hiyo katika tarehe za mbali ili aweze kutafuta nauli ya kujia mahakamani kwa kuwa anatoka mbali mkoani Shinyanga. - Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 9, mwaka huu huku dhamana ya mshitakiwa ikiwa wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho watakaosaini bondi ya Sh milioni tatu. - HabarileoUPDATES