Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hadhi ya Simba ni Ligi ya Mabingwa, sio michuano mingine - Mgunda

Juma Mgunda Sababu.jpeg Juma Mgunda.

Thu, 16 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaimu Kocha Mkuu Simba SC, Juma Mgunda amesema kuwa klabu hiyo ni kubwa hivyo kutokana na ukubwa wake inapaswa kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika na si michuano mingine yoyote.

Mgunda amesema hayo kuelekea mchezo wao wa Ligi dhidi ya Dodoma Jiji ambao utapigwa kesho mjini Dodoma huku Simba ikichuana na Azam FC ili kumaliza katika nafasi ya pili ili wawe na tiketi ya kushiriki Klabu Bingwa msimu ujao

“Tutaingia uwanjani kuikabili Dodoma Jiji kwa lengo la kusaka ushindi ili kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu ujao 2024/25.

"Simba SC ni timu kubwa na inachostahili ni kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika sio michuano mingine, tunaupa uzito mkubwa mchezo huu, tukiweka malengo ya kupata nafasi ya kushiriki michuano hii," amesema Mgunda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live