Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haalubono bado yupo Yanga

Haluubono Haalubono bado yupo Yanga

Sat, 3 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Meneja wa Yanga Princess, Kibwana Matokeo amesema tetesi za kuondoka kwa kocha mkuu Charles Haalubono hazina ukweli.

Tetesi hizo zinakuja baada ya Haalubono kuwa na mwanzo mbaya Ligi Kuu ya Wanawake ambayo kwenye mechi saba imefungwa tatu na kushinda nne na imekuwa ikisemwa mitandaoni kwamba huenda safari ikamkuta punde kama waliomtangulia.

Yanga ilifungwa na watani wao Simba Queens 3-1, JKT Queens 3-1 na kisha kuruhusu kufungwa na Ceasia Queens bao 1-0 mechi zilizopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Akizungumza na Mwanaspoti, kiongozi huyo ambaye pia ni msaidizi wa mkurugenzi wa mashindano klabu ya Yanga, alisema Haalubono anaendelea kukinoa kikosi hicho kwa ajili ya mechi zijazo za ligi.

“Ninachofahamu kocha yupo na anaendelea kukinoa kikosi chetu kwa ajili ya mechi ijayo na Geita Gold Queens,” alisema Kibwana. JKT inaendelea kuongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 18 ikifuatiwa na Simba Queens pointi 16 na ya tatu ikikaa Ceasiaa na pointi 13 ikitofautiana pointi moja na Yanga iliyopo nafasi ya nne.

Chanzo: Mwanaspoti