Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haaland wa Zenji mwenye rekodi tamu Amaan

Haaland Zenji Haaland wa Zenji mwenye rekodi tamu Amaan

Fri, 26 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa soka wa visiwani Zanzibar wamempachika jina la Haaland, wakimfananisha na nyota wa Man City ya England, Erling Haaland kutokana na umbile na kasi yake ya kucheka na nyavu.

Majina yake kamili ni Akram Omar Muhina, nyota wa zamani wa KVZ aliyevuka Bahari ya Hindi kutoka KVZ hadi KMC iliyovutiwa na kipaji chjake kupitia michuano ya Kombe la Mapinduzi 2024.

Nyota huyo aliyemaliza michuano ya Mapinduzi akiwa na mabao mawili, lakini akiandika rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, mjini Unguja ambao umetoka kukarabatiwa na kuwa na muonekano mpya.

Mwanaspoti limefanya mahojiano maalumu na mchezaji huyo ambaye amefichua namna alivyolikatia tamaa soka kabla ya KVZ kumtambulisha na Mapinduzi kumbeba zadi na mwisho kulamba dili la kutoa Ligi Kuu Bara akinyakuliwa na KMC. Endelea naye.

ALIKOANZIA

Safari ya soka la Akram inaanzia kwenye Kituo cha Kulelea Yatima cha SOS Village, kilichopo Mombasa, Mkoa wa Mjini Magharibi baada ya kufiwa na baba mzazi akiwa na umri wa miaka saba tu na alikaa hapo na kupata elimu yake ya msingi humo ndani.

“Sikuwa na ufahamu nzuri, hivyo nilifika darasa la saba tu hapo, nikapelekwa Chuo Cha Ufundi Morogoro nikasoma miaka miwili, wakati nipo SOS Village mle ndani kulikuwa na baba yeye aliyekuwa akitufundisha mpira, hivyo sikupata bahati ya kucheza ngazi za vijana (Central, Junior na Juvenile) kutokana na mazingira ambayo nilikuwa nikikaa,” anasema Akram.

Anasema baada ya kurudi kutoka Morogoro moja kwa moja alijitosa kwenye soka akianziatimu ya Poling Land FC, wakati huo ilikuwa Ligi Daraja la Tatu Wilaya ya Mjini kabla ya kutua Mlandege FC, ambako hata hivyo hakuwa anaapata muda mwingi wa kucheza zaidi ya kukalishwa benchi.

“Nilipokuwa Mlandege, sikupewa nafasi ya kucheza hawakuniamini kabisa, hivyo sikumaliza msimu nikaondoka , nikaenda Gulioni City wakati huo ikiwa Daraja la Pili Wilaya ya Mjini na hapo pia nikaondoka kwenda kujiunga na Mchangani ioliyokuwa Ligi Daraja la Kwanza kabla ya kushuka,” anasema Akram.

Anasema baada ya timu ya Mchangani kushuka alirudi tena Gulioni nikacheza msimu mzima 2020-2021 kabla ya kuibukia Black Sailor iliyokuwa Ligi Kuu ya Zanzibar (ZPL).

Anasema hata hata hivyo mambo hayakumuendea vyema kwani akiichezea timu hiyo msimu wa 2021-2022 Black Sailors, lakini mambo hayakumuendea vyema na kuishia kutolewa kwa mkopo na kurudi tena Gulioni iliyopo Ligi ya Mkoa wa Mjini Magharibi.

Baada ya kurudi tena Gulioni, nayo timu nayo ikashuka daraja hivyo akaamua kuacha mpira kabisa. “Iliposhuka daraja Gulioni nikakosa timu ya kucheza nikaa juu nikasema masuala ya mapira basi, nikaa tu juu nikawa naenda uwanjani kuangalia mechi za ndondo tu,” anasema Akram na kusema hakuwahi kufikiria kama angeweza kurudi kucheza soka kwa changamoto alizokutana nazo.

KVZ WAMBEBA

Anasema hadi sasa huwa haamini kilichoifanya KVZ hata ikamsajili na kuna wakati anaamini ni miujiza tu iliyomtokea na kwa vile kwa Mungu hakuna kinachoshindikana, basi anaishia kushukuru tu.

Straika huyo mrefu na mwenye mwili jumba anasema wakati yupo Uwanja wa Mao anaangalia mechi ya Ndondo, ghafla alishangaa akifuatwa na viongozi wa KVZ wakimwambia wanamhitaji wamsajili katikia timu hiyo.

“Nilishindwa hata kuamini na kubaki najiulizahivi KVZ kweli wananitaka? Nilikuwa siamini niliona kama wananitania, lakini ikawa kweli baada ya kukubaliana nao na siku ya pili baadae kuanza nao mazoezi kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu (ZPL),” anasema.

Akram anasema alitambulishwa rasmi na timu hiyo siku ya Agosti 29, 2023 kuwa ni mchezaji mpya wa KVZ kwa mkataba wa mwaka mmoja na hapo ndipo watu wakaanza kumtambua yeye ni nani, kwani alianza kwa kasi na kuifungia timu hiyo mabao mbali na kutengeneza nafasi kwa wachezaji wenzake.

Anasema mashabiki walivutiwa na umbile alililonalo na kasi yake ya kusumbua mabeki na kumpachika jina la Haaland ambayo ndilo lililozoeleka kwa sasa hara wakati akitua KMC kupitia dirisha dogo la usajili lililofungwa katikati ya mwezi huu.

Anasema mambo yake yalianza kubamba Septemba 6 mwaka jana katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ngome kwa kufunga bao wakati timu hizo zikifungana bao 1-1, kiasi cha kumvutia Kocha Mkuu wa KVZ, Ali Mohammed Ameir na kumpa nafasi zaidi kwenye kikosi hicho.

Akram anasema Ligi Kuu ilipoanza alifanya mambo kwa kuiwezesja KVZ kushinda mabao 3-0 mbele ya JKU akifunga moja ya mabao hayo katika mechi hiyo iliyopigwa Oktoba 12, kisha kufunga mabao mawili walipozamisha New City kwa mabao 4-2 katika mechi iliyopigwa Desemba 9 na kuasisti pia bao moja.

Hadi anaondoka KVZ, Akram ameifungua mabao manne na kuasisti mara tano katika Ligi Kuu Bara kupitia michezo 11.

REKODI TAMU

Haaland huyo wa Zanzibar anasema amefurahi kuandika historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga kwenye Uwanja Mpya wa Amaan, wakati KVZ ikiizamisha Jamhuri kwa mabao 2-0, akifuata nyayo za Abdi Kassim ‘Babi’ aliyefunga kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na Mohammed Khamis ‘Dingo’.

Dingo, ambaye kwa sasa ni marehemu aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga bao kwenye Uwanja wa Amaan mwaka 1971 kwenye mchezo wa ufunguzi wa uwanja huo ambapo aliifungia bao timu yake ya Jeshi ikicheza dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga.

Babi kwa upande wake alifunga bao kwenye ufunguzi wa Kwa Mkapa katika mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Uganda The Cranes mchezo uliiopigwa Septemba 01, 2007.

Ikimbukwe kabla ya mchezo huo wa KVZ na Jamhuri uliopigwa Desemba 29 kulikuwa tayari zimechezwa mechi tatu kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, bila ya kupatikanwa bao lolote, Zanzibar Heroes dhidi ya Kilimanjaro Stars zilizotoka suluhu na michezo miwili ya Kombe la Mapinduzi 2024 kati ya Mlandege na Azam FC na ule wa Chipukizi na Vital’O ya Burundi zilizoshindwa pia kufungana.

“Nilijisikia furaha sana maana nilikuwa natamani kufanya kitu ambacho kitakuwa hakisahauliki kiwe kinakumbukwa mara kwa mara,” anasema mshambuliaji huyo aliyezaliwa miaka 25 iliyopita.

NDOTO ZAKE

Licha ya kucheza kwenye timu mbali mbali, lakini alikuwa hapati kitu chochote maana timu hizo zilikuwa za mtaani hivi hazikuwa na pesa na kwa vile yeye alikuwa bado anajitafuta haikuwa shida kwake.

“Labda Gulioni, ndio nilichukua pesa, lakini pesa yenyewe ilikuwa ndogo tu kwa vile timu za nyumbani nilikuwa nakwenda tu kuwaunga mkono unajua timu za mtaani hazina pesa tofauti na timu za vikosi ,KVZ ndio mambo yalikuwa mazuri,” anasema Akram anayefichua malengo yake kwa sasa ni kubeba taji kwa sababu kwenye timu zote hizo alizopita hajawahi kufanya hivyo.

Anasema anajipanga vizuri kupambania nafasi ya kucheza KMC.

“Kwenye timu lazima ushindani utakuwepo KVZ tulikuwa washambuliaji zaidi ya wanne. Nimejipanga kukabiliana na hiyo hali,” anasema Akram aliyewaomba mashabiki wamuunge mkono.

Chanzo: Mwanaspoti