Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haaland peke yake hawezi kuipa ubingwa Man City

Haaland Vs Newcastle Haaland peke yake hawezi kuipa ubingwa Man City

Wed, 7 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola anakiri uwezo mkubwa wa Erling Haaland unaweza kusaidia Manchester City kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza lakini anasisitiza Mnorway huyo hawezi kufanya hivyo peke yake na kuwa anahitaji ushirikiano wa wachezaji wenzake.

Haaland ambae amesajiliwa na Mancheser City kutoka Borussia Dortmund kwa pauni milioni 51 msimu huu wa joto amekuwa kwenye kiwango bora katika ligi kuu ya Uingereza akifunga mabao 10 katika mechi sita za kwanza za ligi.

Rekodi ya kutisha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ya kufunga mabao 23 katika mechi 19 za Ligi ya Mabingwa Ulaya imechochea maoni kwamba anaweza kuwa nguzo muhimu katika harakati za City kutafuta ubingwa wa Ulaya, lakini Guardiola anasisitiza kwamba matarajio yanapaswa kubebwa na kikosi chake kizima.

“Wachezaji wote ambao klabu iliamua kuwasajili msimu huu walikuja kujaribu kutufanya kuwa bora zaidi la sivyo haitakuwa na maana,” Guardiola alisema.

“Je, msaada huo utatusaidia kushinda taji? Sijui. Siku zote nina imani, lakini tukitegemea mabega ya Erling tu, hatuwezi kushinda Ligi ya Mabingwa. Tunachopaswa kufanya ni kucheza vizuri, tengeneza nafasi za kumsaidia kufunga mabao na tunatumai tunaweza kufanya hivyo”

“Natumai anaweza kutusaidia lakini hatutashinda kwa ajili ya Erling pekee, hizi ni hisia zangu. Ana ubora wa kipekee na katika michezo muhimu labda anaweza kutatua matatizo tuliyo nayo, lakini tusipocheza vizuri hatutashinda mechi katika Ligi ya Mabingwa au Ligi Kuu.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live