Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haaland ni mwendo wa bata tu

Haaland Bata Tu 18941230

Sat, 15 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Fainali za Euro 2024 zinaendelea huko Ujerumani, lakini straika Erling Haaland amechagua namna nyingine ya kujiweka mbali na soka baada ya kuonekana akiponda raha kwenye boti za kifahari huko Cannes, Ufaransa.

Baada ya purukushani za kutosha kwenye mikikimikiki ya soka kwa msimu uliopita, straika huyo wa kimataifa wa Norway, amepata nafasi ya kuanza mapumziko mapema kutokan na timu yake ya taifa kushindwa kufuzu fainali za Euro 2024, hivyo anachofanya kwa sasa ni kuponda tu raha.

Staa huyo wa Manchester City, Haaland, 23, alionekana kwenye boti ya kifahari akiwa na marafiki zake, huku akicheza mpira wa kucheza kwenye maji, kabla ya kuonekana pia akiendeesha pikipiki za kwenye maji.

Kwenye boyi hiyo, Haaland alikuwa na marafiki zake pamoja na baba yake mzazi, Alfie, 51, ambaye ni staa wa zamani wa Man City na Leeds United.

Erling ameshinda taji la Ligi Kuu England mara mbili, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu yake miwili aliyokuwa kwenye kikosi cha Man City kinachonolewa na Mhispaniola, Pep Guardiola.

Msimu uliopita alifunga mabao 45 katika michuano yote aliyochezea Man City na mabao sita kati ya 14 aliyofunga akiwa na kikosi cha Norway, alifanya hivyo kwenye mechi za kufuzu mikikimikiki ya Euro 2024. Hata hivyo, mabao hayo hayakutosha kuipa Norway tiketi ya kwenbda kushiriki fainali hizo za Ujerumani zilizoanza usiku wa jana Ijumaa. Kwa kifupi, Norway haijafuzu michuano mikubwa tangu 2000.

Mapema wiki hii, Erling alionekana na kujifanya DJ huko Marbella.

Chanzo: Mwanaspoti