Premier League ndio ligi yenye ushindani mkubwa duniani. Ubora wa ulinzi, ushambuliaji na karibu kila nyanja ya soka iko katika kiwango cha juu zaidi.
Baadhi ya wachezaji hufanikiwa kuvuka viwango hivyo na kujikuta wakihusika katika mabao mengi (mabao&asisti).
Leo tunaangalia wachezaji 10 bora wa Premier waliotoa mchango wa mabao mengi zaidi mwaka 2023. Takwimu hazihusishi mechi za juzi wikiendi.
Bukayo Saka – 19 Nyota wa Arsenal, Bukayo Saka ni mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani. Kijana huyo alianza kama kijana anayejitahidi na mwenye uwezo mkubwa na sasa anaanza kuishi kulingana na hilo.
Saka ana mchango wa mabao 19 mwaka huu kwenye Premier. Saka amejidhihirisha ni mchezaji wa kiwango cha dunia akikiwasha dhidi ya timu kubwa kama vile Manchester City, Liverpool, Manchester United na Tottenham Hotspurs pia.
Mwaka unapoisha, Saka anaweza kuongeza idadi yake kama Arsenal akiwa katika kiwango kizuri.
Callum Wilson – 19 Callum Wilson amefanikiwa kufunga mabao 4 ya Premier League katika mechi 6 msimu huu. Amechangia mabao 19 Premier pale Newcastle mwaka 2023. Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anapambana mara kwa mara ili kuanza kikosi cha kwanza na Alexander Isaka.
Harry Kane – 19 Harry Kane kwa sasa amejiunga na wababe wa Bundesliga, Bayern Munich. Ipo wazi Kane bado yuko kwenye orodha licha ya kutocheza Premier tangu miezi 2 iliyopita na hii inaonyesha ni namna gani alivyokuwa mkali.
Harry Kane bila shaka ni mmoja wa washambuliaji bora wa kizazi chetu na pia mchezaji bora wa Tottenham katika miaka michache iliyopita.
Harry Kane sio tu mshambuliaji bali pia ni hodari wa kupiga pasi. Upigaji pasi wake pamoja na uwezo wake wa kufunga mabao ulimfanya kuwa mshambuliaji bora kwenye Premier pamoja na Erling Haaland.
Kwa ujumla, msimu uliopita wa Kane kwenye Ligi Kuu alitupia mabao 33 katika mechi 38. Kwa mwaka huu hadi anaondoka alikuwa amehusika kwenye mabao 19.
Ollie Watkins – 21 Bila shaka mchezaji anayechukuliwa poa sana kwenye orodha hii. Ollie Watkins alianza kutengeneza vichwa vya habari na akapata umaarufu baada ya kutua Aston Villa.
Ollie alifanikiwa kuhusika kwenye mabao 15 katika kipindi kilichosalia cha msimu wa 2022-23. Kufikia msimu wa 2023-24, Ollie Watkins hivi majuzi alifunga hat-trick na kutoa asisti dhidi ya Brighton.
Kwa jumla, ana mchango mkubwa wa mabao 22 mwaka 2023 kwa Aston Villa kwenye Premier. Watkins anaonekana kuwa mchezaji muhimu kwani Aston Villa sasa wako nafasi ya 5 kwenye msimamo wa ligi.
Mohammad Salah – 27 Salah amefunga mabao 27 katika Premier mwaka huu pekee. Baada ya kuondoka Sadio Mane pale Liverpool, The Scousers walipoteza mtu muhimu katika safu yao ya ushambuliaji.
Licha ya hayo Salah alionyesha kuwa anaweza kufanya hivyo akiwa hapo bila Sadio Mane pembeni yake. Utendaji bora wa Liverpool mwaka 2023 ulikuja dhidi ya wapinzani wao Manchester United. Vijana wa Klopp waliwazaba United mabao 7.
Katika mechi hiyo iliyokuwa ya upande mmoja, Salah alifunga mabao 2 akisaidia upatikanaji wa mengine mawili. Kwa ujumla, Salah amefanikiwa kukusanya mabao 27 mwaka huu.
Kati ya hayo, Salah ameweza kufunga mabao 3 akisaidia mara 4 katika mechi 7 alizoichezea Liverpool msimu wa 2023-24.
Erling Haaland – 29 Nani mwingine isipokuwa Erling Haaland. Raia huyo wa Norway amevunja rekodi nyingi katika msimu wake wa kwanza akiwa na Manchester City. Uwezo wake wa juu, ufahamu wa nafasi na umaliziaji wake ni wa kiwango cha kimataifa kabisa.
Kwa ujumla, Erling Haaland amefanikiwa kuhusika kwenye mabao 29 katika Premier kwa mwaka 2023. Salah pekee ndiye anayekaribia kumpita mwaka unapoisha. Kufikia msimu huu, Haaland haonyeshi dalili za kuacha kufunga, tayari ameingia nyavuni mara nane na asisti moja katika mechi 7 za Premier.
WENGINE Bruno Fernandes – 15 Marcus Rashford – 15 Son Heung Min – 17 Bryan Mbuemo – 18.