Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haaland mchezaji Bora Norway akimgaragaza kiungo wa Arsenal

Haaland Norway.jpeg Erling Braut Haaland

Thu, 26 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Manchester City raia wa Norway, Erling Haaland amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Norway baada ya kuwa na msimu mzuri akiwa na Man City katika michuano tofauti msimu huu.

Haaland anashinda Tuzo hiyo kwa mara ya tatu mfululizo kufuatia kiwango bora anachoonesha akiwa na klabu ama Timu ya Taifa.

Haaland ananyakua tuzo hiyo akimpiku kiungo wa Arsenal Martin Odegaard aliepata kuchukua tuzo hiyo mwaka 2019.

Haaland ndio kinara wa ufungaji Ligi Kuu ya England akiwa ameshapachika mabao 25 mpaka sasa ikiwa ndio kwanza nusu ya kwanza ya msimu imemalizika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live