Sun, 26 Mar 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Baada ya Real Madrid kuonesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo, Manchester City inataka kuboresha mshahara wake mpaka Tsh bilioni 1.4 kwa wiki ili kumshawishi abaki.
Haaland (22) ambaye amefunga magoli 42 katika michuano yote msimu huu, ana mkataba hadi Mwaka 2027
Kwa sasa, Haaland analipwa Paundi 375,000 kwa wiki akiwa sawa na Kevin De Bruyne wa Man City na kipa wa Man United, David de Gea, hivyo akiboreshewa mshahara na kuwa Paundi 500,000 itamaanisha atakuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa katika Premier League.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live