Erling Haaland ameweka rekodi baada ya kufunga mabao matano ndani ya dakika 35 dhidi ya RB Leipzig usiku wa kuamkia jana na hivyo kumfanya awe amefikisha mabao 39 katika mechi 35.
Rekodi hiyo aliweka kwenye raundi ya 16 bora ya Ligi Mabingwa Ulaya Man City ikitinga robo fainali ya michuano hiyo ikiichapa RB Leipzig mabao 7-0.
Vile vile Haaland akavunja rekodi ya muda wote ya Man City iliyokuwa imewekwa na Tommy Johnson miaka 94 iliyopita.
Haaland, aliyekuwa hatari kwenye mchezo huo dhidi ya Leipzig, alifunga hat-trick kwenye kipindi cha kwanza, ikiwa ni hat-trick yake ya tano msimu huu.
Haaland amefikisha mabao tisa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya huku akiweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefikisha mabao 30 kwa haraka zaidi katika michuano hiyo.
Haaland amepiku rekodi ya Ruud van Nistelrooy, ambaye alifikisha mabao 30 katika mechi 34, wakati yeye akifikisha idadi hiyo ya mabao baada ya kucheza mechi 25 tu. Haitoshi Haaland amelingana na wakongwe wengine, Wayne Rooney aliyefunga mabao 30 katika mechi 85, mwingine ni Samuel Eto'o na Kaka. Aidha Kaka na Etoo walihitaji mechi 55 kila mmoja kufikisha idadi ya mabao 30. wenyewe walihitaji mechi 55 kila mmoja kufikisha idadi hiyo ya mabao 30.
Wakati huo huo Haaland amekuwa mchezaji mdogo zaidi kwenye historia ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kufikisha mabao 30.