Erling Haaland ameweka rekodi ya namna yake England kwa kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Ligi Kuu England kufikisha haraka bao 30.
Rekodi imeandikwa kufuatia mchezaji huyo kufunga magoli mawili kwenye ushindi wa bao 4-1 walioupata Manchester City dhidi ya kibonde Southampton.
Ushindi ambao Manchester City wameupata umepunguza pengo la pointi dhidi ya timu iliyonafasi ya kwanza Arsenal kufikia tano ingawa Washika Mtutu hao watacheza Liverpool Jumapili.
Haaland, alitumia pasi ya Jack Glealish kufunga bao la kwanza kabla ya kuongeza bao la pili na kufanya kufikisha goli 30 kwenye mechi 27 za EPL.
Sasa Haaland amefunga magoli 44 kwenye mashindano yote.
Mabao mengine yakafungwa na Glealish, na Julian Alvarez likiwa ni bao la penati wakati bao la kufutia machozi kwa Southampton likiwekwa kimiani na Sekou Mara.