Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haaland awatumia ujumbe mzito Man United

Haaland Vs United Haaland awatumia ujumbe mzito Man United

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Straika, Erling Haaland ameandika historia baada ya kufunga mabao matano katika mashuti yake saba aliyopiga wakati Manchester City ilipoizabua Luton Town mabao 6-2 katika mchezo wa raundi ya tano ya Kombe la FA uliopigwa usiku wa juzi Jumanne.

Katika mechi hiyo, kiungo mshambuliaji wa Man City, Kevin De Bruyne aliasisti mara nne.

Lakini, ni Haaland aliyeingia kwenye vitabu vya rekodi baada ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Man City tangu mwaka 1926 kufunga mabao matano katika mchezo mmoja wa Kombe la FA.

Frank Roberts ndiye mchezaji wa Man City aliyewahi kufanya hivyo karibu miaka 100 iliyopita, ambapo alifunga mabao matano katika ushindi wa 11-4 dhidi ya Crystal Palace.

De Bruyne aliasisti mabao manne ya kwanza ya Haaland, huku bao la tano la straika huyo wa Norway alifunga baada ya pasi ya Bernardo Silva, wakati ushindi huo ulihitimishwa kwa bao la Mateo Kovacic kufutia pasi kutoka kwa beki John Stones.

Mabao hayo matano ya Haaland yanamfanya awe amefunga mara 27 katika mechi 29 alizocheza msimu huu.

Huenda akashindwa kufikia kiwango cha msimu uliopita, ambapo alifunga mabao 52 katika mechi 53, lakini kama ataendelea kwa kasi yake ya kutupia kama alivyowafanya Luton, basi anaweza kukaribia.

Katika mchezo wa Chelsea, Haaland alikosa nafasi tisa za kufunga, lakini Luton walikuwa kwenye bahati mbaya baada ya kuruhusu nyavu zao kuguswa mara tano baada ya mashuti saba tu ya straika huyo mwili jumba.

Haaland ameanza kufunga bao nyingi wakati akijiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu England, ambapo watakipiga na Manchester United, Jumapili hii kwenye Ligi Kuu England, kisha watacheza na Copenhagen kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya katikati ya wiki ijayo, kisha wataifuata Liverpool huko Anfield.

Alichokifanya Haaland ni kama onyo kwa mahasimu wao Man United, ambao watawakaribisha kwenye Uwanja wa Etihad saa 12:30 jioni Jumapili hii katika mechi yao ya Ligi Kuu England.

Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana kwenye Uwanja wa Etihad, Manchester United ilichakazwa 6-3 katika mechi Na. 188 ya Manchester Derby, ambako Haaland na Phil Foden kila mmoja alifunga ‘hat-trick’.

Chanzo: Mwanaspoti