Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haaland avunja rekodi ya Nistelrooy, Salah England

Haalnda Vs Sala Van Haaland anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao mengi ndani ya msimu mmoja kutoka England

Wed, 12 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland amefikisha magoli 45 mpaka sasa msimu huu kwenye michuano yote. Idadi hiyo ya magoli haijawahi kufikiwa na mchezaji yeyote wa klabu ya Ligi kuu England kihistoria.

Haaland amevunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na Ruud van Nistelrooy (Man Utd 2002/03) na Mohammed Salah (Liverpool 2017/18) ya magoli 44 kila mmoja.

Magoli mengi zaidi kwa mchezaji wa Ligi kuu England kihistoria

45 - Erling Haaland (22/23) 44 - Ruud van Nistelrooy (02/03) 44 - Mohamed Salah (17/18)

Haaland alifunga bao moja katika ushindi wa Manchester City wa 3-0 dhidi ya Bayern Munich katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya siku ya Jumanne usiku.

Mabao mengine ya Man City yalifungwa na Rodrigo na Bernardo Silva ambaye Kila mmoja amefunga bao moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: