Mchezaji wa Manchester City Erling Haaland ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Wanaume ya PFA, huku Bukayo Saka wa Arsenal akitangazwa kuwa Mchezaji Bora Chipukizi wa Mwaka.
Mshambuliaji wa Norway Haaland, 23, alifunga mabao 52 katika mashindano yote katika msimu wake wa kwanza akiwa na kikosi cha Pep Guardiola.
Haaland aliwashinda wachezaji wenzake Kevin de Bruyne na John Stones, Saka wa Arsenal na Martin Odegaard na Harry Kane wa Tottenham, sasa yuko Bayern Munich.
City ilishinda Ligi ya Primea, Kombe la FA na Ligi ya Mabingwa msimu uliopita.
"Ni heshima kushinda tuzo hii ya kifahari," alisema Haaland. "Kutambuliwa na washindani wako ni jambo nzuri na ningependa kumshukuru kila mtu aliyenipigia kura.
"Ulikuwa msimu usiosahaulika kwa timu na kwangu binafsi. Kushinda mataji matatu ilikuwa kitu ambacho sikuwahi kufikiria, kwa hivyo kufikia hilo na kundi maalum la wachezaji ilikuwa hisia ya kushangaza.