Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haaland arejea na magoli yake Dortmund, afunga moja wakiichapa Wolfsburg 3

FFOk2u3WQAIBzd Erling Braut Haaland arejea baada ya kupona majeraha

Sat, 27 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji hatari kwa sasa ulimwenguni, Erling Haaland amefunga goli wakati akirejea uwanjani baada ya kuwa nje kwa takribani mwezi mmoja alipokua akisumbuliwa na majeraha.

Dortmund ilitoka nyuma na kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 jioni ya leo dhidi ya VfL Wolfsburg katika mchezo wa Bundasliga.

Mshambuliaji huyo raia wa Norway, amefunga katika dakika ya 81 baada ya kuingia kipindi cha pili akitokea benchi kufuatia kutengemaa kwa majeraha yaliyokuwa yakimkabili ya misuli ambayo yalimueka nje tangu kati kati ya mwezi Oktoba.

Ukiwa ni ushindi wao wa sita katika mechi saba zilizopita, umewafanya Dortmund kufikisha alama 30, alama moja nyuma ya vinara wa Bundasliga Bayern Munich ambao nao leo wameibuka na ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Arminia Bielefeld.

Wababe hao wa Bundasliga wanakwenda kukutana mwishoni mwa juma lijalo.

"Mengi yametokea siku chache zilizopita, lakini cha msingi leo tumecheza mchezo mzuri na matokeo yanajieleza" amesema mchezji wa Dortmund Julian Brandt

Dortmund wametolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya siku ya Jumatano na Sporting Lisbon baada ya kukubali kichapo cha magoli 3-1.

"Tuna furaha kupitiliza,na tuna wiki nzima ya kujianda kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Bayern na tutakwenda huku tukiwa tunajiamini" amesema.

Magoli mengine ya Dortmund yamefungwa na Emre Can kwa panati na D. Malen, wakati lile la Wolves limefungwa na Wout Weghorst dakika ya pili ya mchezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live