Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haaland amshangaza bosi Man City

Haaland X Young Boys Haaland amshangaza bosi Man City

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Manchester City Pep Guardiola amekiri, Mshambuliaji Erling Haaland anaendelea kumshangaza baada ya kuonyesha kiwango cha kuvutia zaidi katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Young Boys uliochezwa juzi Jumanne (Novemba 07).

Licha ya kufunga bao lake la 66 na 67 katika mechi yake ya 70 kwa timu hiyo, Guardiola alisema bado anashangazwa na kipaji alichonacho wakati wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Bosi huyo alisema: “Ndiyo bado ananishangaza, kwa sababu kawaida hufunga mabao katika eneo la yadi sita, ya nane na kwa Penati. Lakini ana kipaji hiki, si mara ya kwanza kufanya hivyo.

“Nadhani pasi ya Rico Lewis ilikuwa ya kushangaza. Ninapenda anaposhambulia katika nafasi ya tatu ya mwisho. Mwendo kutoka kwa mpinzani, udhibiti na ana bao hapa.

“Ana bao katika nafasi hiyo wakati hafikirii sana na upigaji wake ni wa ajabu. Ndio, ilikuwa bao la ajabu. Bao la Phil Foden pia lilikuwa la kushangaza.”

Ushindi huo mzuri kwenye Uwanja wa Etihad uliwafanya vijana wa Guardiola wasonge mbele na kutinga hatua ya mtoano huku kukiwa na michezo miwili imebakia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live