Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haaland aitabiria makubwa Senegal Kombe la Dunia Qatar

OQ TALKSPORT MANE HAALAND Haaland na Mane

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa klabu ya Man City, Erling Haaland amesema kuwa timu ya Taifa ya Senegal itafanya vizuri sana katika Mashindano ya Kombe la Dunia mwaka huu yatakayoanza Novemba 20 nchini Qatar.

Halaand amesema timu hiyo itafanya vizuri kutokana na kuwa na Wachezaji wengi na wenye uzoefu mkubwa akiwepo Sadio Mane ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani.

"Nafikiri Senegal watafanya vizuri sana kombe la Dunia, wana timu nzuri sana yenye wachezaji wengi wenye uzoefu,nadhani itakuwa timu bora ya Afrika katika Kombe la Dunia."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live