Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haaland aipa Man City alama tatu muhimu

Haaland Vs Palace Pen.jpeg Haaland akishangilia bao lake alilofunga kwa mkwaju wa Penati

Sun, 12 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bao pekee la Erling Haaland dakika ya 78 kwa penalti limeipa Manchester City ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Crystal Palace katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa Jumamosi Uwanja wa Venue Selhurst Park Jijini London.

Kwa ushindi huo, Manchester City inafikisha pointi 61 katika mchezo wa 27, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi mbili na vinara, Arsenal ambao pia wana mechi moja mkononi.

Kwa upande wao Crystal Palace wanabaki na pointi zao 27 za mechi sasa nafasi ya 12.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live