Kumekuwa na imani kuwa Mshambuliaji wa Manchester City, Haaland na Mbappe ndiyo wapinzani halisi watakaorithi kiti cha ‘Enzi’ cha Messi na Ronaldo kwenye ushindani kama mchezaji mmoja mmoja lakini pia kwa kuzipatia mafanikio timu zao.
Hata hivyo, Haaland amefunguka kuhusu kushindanishwa na Mbappe na kudai kuwa anajiangalia binafsi.
“Lakini kamwe sijawahi kujizungumzia mwenyewe kwa kujishindanisha dhidi ya mchezaji mwingine, sio njia ya kuona vitu. Nipo bize na mambo yangu, najaribu kuwa bora kila siku, kuendelea kufurahia kile ninachofanya na kuwa bora katika maono yangu.”
Mapema mwezi huu Erling Haaland alitajwa kama Mchezaji Bora wa mwakwa wa UEFA kwa upande wa wanaume kufuatia kuwa na msimu mzuri na Klabu yake ya Manchester City.
Haaland pia ametajwa kwenye kinyang’anyiro cha tuzo ya Ballon d’Or wakati bado ana umri mdogo wa miaka 23.