Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haaland aendelea kutupia, City ikichukua alama tatu

Haaland Scored Two Goals.jpeg Haaland amefunga magoli mawili mchezo dhidi ya Brighton

Sun, 23 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa EPL, Manchester City wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Brighton & Hove Albion katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Uwanja wa Etihad.

Mabao ya Man City yalifungwa na Erling Haaland mawili dakika za 22 na 43 kwa penalti na Kevin De Bruyne dakika ya 75, wakati la Brighton limefungwa Leandro Trossard dakika ya 53.

Kwa matokeo hayo, Manchester City wanafikisha pointi 26 katika mchezo wa 11, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi moja na vinara, Arsenal ambao pia wana mechi moja mkononi.

Kwa upande wao, Brighton & Hove Albion wanabaki na pointi zao 15 za mechi 11 pia nafasi ya nane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live